MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR NI KICHOCHEO MAENDELEO YA KISWAHILI ULIMWENGUNI
Ikiwa imepita miaka 48 tangu Tanganyika na Zanzibar ziungane na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala yanayozungumziwa sana katika Muungano huu kwa sasa ni masuala ya Katiba Mpya na Siasa. Tumesahau kwamba Muungano huu ndiyo uliozaa Jamhuri na kuitengeneza hiyo Katiba ambayo hii leo imeundwa Tume ya kupitia maoni ya Watanzania ili kupata Katiba Mpya.
Ikiwa imepita miaka 48 tangu Tanganyika na Zanzibar ziungane na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala yanayozungumziwa sana katika Muungano huu kwa sasa ni masuala ya Katiba Mpya na Siasa. Tumesahau kwamba Muungano huu ndiyo uliozaa Jamhuri na kuitengeneza hiyo Katiba ambayo hii leo imeundwa Tume ya kupitia maoni ya Watanzania ili kupata Katiba Mpya.
Jambo la kukumbuka ni namna lugha yetu adhimu ya
Kiswahili ilivyotumika kama . Ni Kiswahili ambacho ndicho kilileta changamoto
za muungano huu kwani wa leo hii. Tukumbuke kwamba Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati
Aman Abeid Karume walitumia Kiswahili katika kuuunganisha watu wa mataifa haya
mawili na kuwa kitu kimoja kama Watanzania.
Leo hii mifumo yetu ya elimu inaonyesha haikipi
nafasi Kiswahili kwa upana wake. Kiswahili kinachukuliwa ni lugha ya kishamba
na kuzitukuza lugha za kigeni kama vile Kiingereza na Kifaransa. Watu
hulazimika hata kutoa pesa nyingi ili tu waweze kuzijua lugha hizo na kusahau
umuhimu wa lugha yao. Hivi huku ndiyo kukitangaza Kiswahili au kukididimiza?
Kwa nini hatuna uzalendo na lugha yetu. Vijana wengi
utawakuta hata kwenye mazungumzo yao ya kawaida wanatumia zaidi Kiingereza
ambacho nacho ni kibovu. Kila mtu anataka aonekane kwamba anakijua zaidi ya mwenzake.
Kwani ukizungumza lugha yako haueleweki? Mtu yupo radhi achanganye misimbo ili
mradi tu. Tumekua watu wa kuthamini
tusichonacho kuliko kile tulichonacho.
Jamii hivi sasa imeathirika na wengi tunakichukulia
Kiingereza kama lugha ya wasomi. Hii ni dhahiri kwa watu wengi ambao wakifika
majumbani kwao hasa wa sehemu za vijijini hawatumii tena hata zile lugha zao za
asili kwa kuwa ametoka masomoni, hivyo kutafuta utofauti kati yake na watu
aliowakuta huko. Anachotaka yeye ni ile hali ya kujiona amesoma kuliko mtu
yeyote hapo kijijini.
Kwa nini
tunasahau tulipotoka. Sisi ni Watanzania na tuliamua kwa pamoja kukitumia
Kiswahili kama Lugha ya Taifa. Sasa inakuaje tukidharau. Hatuoni kama tunajidharau
wenyewe na kukiona Kiswahili kama si cha kwetu Watanzania. Ina maana maamuzi
tuliyoyachukua na kuamua kukifanya Kiswahili kuwa lugha yetu ya Taifa tulikosea
au tulilazimishwa. Sidhani kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
alipitisha kuwa Lugha ya Kiswahili itumike kama Lugha ya Taifa alikosea!. Kama
kulikuwa na watu wa kupinga mbona hawakujitokeza wakakubaliana na matakwa
yaliyotolewa. Leo hii tunavyokidharau inamaanisha kuwa Kiswahili hakina haja ya
kuendelezwa? Tafakari!
Mwandishi ni
mtaalamu wa lugha.